16 Septemba 2025 - 16:25
Amir Pourdastan: Moyo wa taifa la Iran unapaswa kujitolea kwa vikosi vya jeshi

Mkuu wa Kituo cha Tafiti za Kimkakati cha Jeshi alisema: Wananchi wa Iran wawe na moyo thabiti na wawe na utulivu, na wafahamu kuwa watoto wao na ndugu zao walioko jeshini wana ujuzi na maandalizi ya kutosha.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-: Amir Sarlashkar Ahmadreza Purdastan, Mkuu wa Kituo cha Tafiti za Kimkakati cha Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, katika mahojiano, akizungumzia vita vya siku 12, alisema:

"Wananchi wa Iran wafahamu kuwa vikosi vya ulinzi, licha ya vikwazo vilivyodumu kwa miaka 46, vimesimama imara dhidi ya dunia ya ubeberu, na wamewalazimisha wanyanyasaji wa Kimarekani, Kizayuni na wa Magharibi kusalimu amri."

Aliongeza kuwa:

"Katika vita hivyo vya siku 12, wanajeshi na viongozi wa kisiasa wa adui walinyanyua mikono yao kuashiria kusalimu amri na waliomba kusitisha mapigano (sitisho la vita), jambo ambalo linaonesha nguvu, uwezo na uimara wa vikosi vya ulinzi vya Iran."

Mkuu huyo aliendelea na kusema:

"Wananchi wa Iran wawe na hakika kwamba ikiwa adui atathubutu kuchukua hatua yoyote, atakabiliwa na jibu kali litakalomletea majuto."

Aliongeza kuwa:

"Katika vita vya siku 12, tulipambana na adui hasa kwa kutumia makombora, lakini katika vita vijavyo, iwapo itahitajika, tutamkabili adui katika nyanja nyingine pia, na tutaionesha dunia uwezo wa askari wa Imam Khamenei (Mwenyezi Mungu amhifadhi) na askari wa Kiislamu."

Purdastan pia alizungumzia jukumu la sanaa katika kuonesha nguvu ya vikosi vya ulinzi:

"Wasanii wetu wameingia katika nyanja mbalimbali kama filamu na muziki. Mfano wake ni wimbo 'Alaj' ulioimbwa na Mohsen Chavoshi, pamoja na filamu za hali halisi (documentaries) zenye nguvu zilizotengenezwa. Wasanii wengine pia wanaweza kushiriki kwa kuunga mkono vikosi vya ulinzi, ili kuongeza motisha na ari yao."

Katika hitimisho, Mkuu huyo alisema:

"Nikiwa kama askari, nasema: wananchi wa Iran wawe na moyo thabiti na wawe na utulivu, na wafahamu kwamba watoto na ndugu zao walioko jeshini wana maandalizi ya kutosha."

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha